Boitique

Boitique

Tuesday 10 September 2024

Mkutano wa Kimataifa wa Akili Bandia (GAIN) kufanyika Riyadh, Saudi Arabia

 

H.E. Mr. Yahya bin Ahmed Okeish - Ambassador of the Kingdom of Saudi Arabia to the United Republic of Tanzania.



Kuwaleta pamoja zaidi ya viongozi 300 wa Akili Bandia duniani



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKUTANO wa Kimataifa wa Akili Bandia (Global AI 2024) unaoandaliwa na Mamlaka ya ya Saudia ya Akili Bandia (SDAIA) unatarajiwa kufanyika mjini Riyadh, Saud Arabia Septemba 10 mpaka 12 huku ukitarajiwa kuwaleta pamoja viongozi zaidi ya 300 wa akili bandia.

 

Mkutano huo unatarajiwa kuwa na moja ya mikusanyiko muhimu zaidi katika Akili Bandia mwaka huu ambapo jana mamlaka hiyo imetangaza safu yake ya wazungumzaji wakuu.

 

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Balozi wa Saudi Arabia hapa nchini, Yahya Bin Ahmed Okeish imesema mkutano huo ambao unaenda sambamba na Dira ya Saudi Arabia ya 2030 inayolenga kuleta uchumi mchanganyiko, umeandaliwa ili kukuza ushirikiano wa kimataifa na kuangalia uwezekano wa kuleta mabadiliko ya Akili Bandi katika sekta mbalimbali.

 

“Mijadala ya wazungumzaji zaidi ya 300 wakiwemo wavumbuzi, wasomi, watendaji, wadhibiti na watoa maamuzi kutoka nchi 100 duniani kote itazingatia Kaulimbiu ya mkutano huo isemayo "Sasa, ifuatayo, Kamwe". Ilisema taarifa hiyo.

 

Aidha taarifa hiyo imeelza kuwa vikao vitajadili athari za mabadiliko ya teknolojia kwa watu na jamii, faida halisi inayopata dunia kutokana na Akili Bandia, mwelekeo wa teknolojia wa siku zijazo na umuhimu wa kuzingatia maadili ili kuhakikisha kuwa uwajibikaji wa maendeleo ya Akili Bandia unakuwa katika sekta zote.

 

Mkutano huo utajumuisha safu ya kuvutia ya wazungumzaji wa kimataifa ikiwa ni pamoja na Cristiano Amon ambaye ni Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Qualcomm Incorporated, Nick Studer, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oliver Wyman Group, Dk. Marc Raibert ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Boston Dynamics, Marcelo Claure ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Claure Group na Julie Sweet ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Accenture.

 

Wengine ni Amandeep Gill, Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Teknolojia, Kathleen Kennedy ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha MIT cha akili ya pamoja, Alex Smola ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Boson AI, Andrew Feldman, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Cerebras Systems, Dk. Chris Miller, Mkurugenzi wa kampuni ya Greenmantle na Caroline Yap, Mkurugenzi Mkuu wa Kimataifa kutoka kampuni ya Google Cloud.

 

Taarifa hiyo imewataja wengine kuwa ni Stefan Schnorr ambaye ni Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala Dijitali na Uchukuzi ya Shirikisho la Ujerumani, Charles-Edouard Bouée, Mwanzilishi Mwenza na Mshirika Msimamizi wa kampuni ya Adagia), Jonathan Ross ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Groq na Dk. Deepak Chopra ambaye ni Mwanzilishi wa taasisi Chopra.

 

Wakati huohuo Msemaji Mkuu wa Mamlaka ya Saudi Arabia ya Akili Bandia (SDAIA), Mhandisi Majed Al-Shehri, amesema mkutano wa Kimataifa wa Akili Bandia utakuwa ni tukio la kihistoria katika kuunda mustakabali wa Akili Bandia na kwamba Kaulimbiu ya “Sasa, Ijayo, Kamwe” ni muhimu sana kwani inawapa changamoto ya kuangalia athari za haraka, uvumbuzi wa siku zijazo, na majukumu ya kimaadili yanayokuja na maendeleo ya haraka ya teknolojia ya Akili Bandia.

 

“Hii ni teknolojia ambayo inatia matumaini sana, lakini tunapovumbua, pia hatuwezi kumudu kuikosea. Ni muhimu kwamba ushirikiano wa Akili Bandia uwe endelevu na kwa ajili ya kuboresha jamii. Ushiriki mkubwa wa viongozi wa kimataifa, haswa kutoka katika tasnia ya ushauri unaonesha jukumu muhimu la Akili Bandia katika mabadiliko ya biashara na uvumbuzi wa kimataifa na kujitolea kwao kwa ushirikiano katika kipindi ambacho tunatafuta namna ya kutatua maswali mengi ambayo teknolojia hii inayaibua." Alisema.

 

- MWISHO -


Global AI Summit (GAIN) to be held in Riyadh, Saudi Arabia

H.E. Mr. Yahya bin Ahmed Okeish - Ambassador of the Kingdom of Saudi Arabia to the United Republic of Tanzania.


The summit is set to bring together more than 300 AI leaders


By THE GUARDIAN Reporter

DAR ES SALAAM

MORE than 300 Artificial Intelligence leaders are expected to participate in the Global AI Summit 2024 hosted by the Saudi Data & Artificial Intelligence Authority (SDAIA) to be held in Riyadh, Saudi Arabia in September 10 to 12.

 

The summit is set to be one of the most important gatherings in AI this year and yesterday announced its line-up of headline speakers. The summit, which aligns with Saudi Arabia's Vision 2030 to diversify the economy, is designed to foster global collaboration and explore the transformative potential of AI across industries.

 

According to the statement issued by the Ambassador of the Kingdom of Saudi Arabia to the United Republic of Tanzania in Dar es Salaam Mr. Yahya bin Ahmed Okeish yesterday said the deliberations of over 300 speakers, including innovators, academics, executives, regulators and decision-makers from 100 countries worldwide, will be centered around the summit’s theme: "Now, Next, Never".

 

The statement said sessions will discuss technology’s transformative impact on people and communities, the real world benefits of AI, the technology’s future trajectory and the ethical considerations necessary to ensure responsible AI development across all sectors.

“As we approach the third edition of the Global AI Summit, we stand poised at the threshold of a new era, where AI's transformative power will be harnessed to explore AI through the lens of 'Now, Next, never examining the current state of AI, its future trajectory, and the ethical considerations necessary to ensure a desirable future. A future where the need for international collaboration to fully harness AI’s potential and manage its impact responsibly has never been more urgent.” The statement elaborated.

The summit will feature an impressive line-up of global speakers including Cristiano Amon (President & CEO, Qualcomm Incorporated), Nick Studer (President & CEO, Oliver Wyman Group), Dr. Marc Raibert (Chairperson, Boston Dynamics), Marcelo Claure (Founder & CEO, Claure Group), Julie Sweet (CEO, Accenture), Amandeep Gill (Secretary-General’s Envoy on Technology, United Nations), Kathleen Kennedy (Executive Director, MIT Center for Collective Intelligence) and Alex Smola (CEO, Boson AI).

 

Others are Andrew Feldman (Founder & CEO, Cerebras Systems), Dr. Chris Miller (Director, Greenmantle), Caroline Yap (Global Managing Director, Google Cloud), Stefan Schnorr (State Secretary, German Federal Ministry for Digital and Transport), Charles-Edouard Bouée (Co-Founder & Managing Partner, Adagia Partners), Jonathan Ross (Founder & CEO, Groq) and Dr. Deepak Chopra (Founder, Chopra Foundation).

 

Meanwhile, SDAIA's official spokesperson Eng. Majed Al-Shehri said the Global AI Summit will be a landmark event in shaping the future of AI-Shehri said the theme 'Now, Next, Never' is especially pertinent as it challenges them to consider the immediate implications, future innovations, and the ethical responsibilities that come with the rapid advancement of AI technologies.

 

He added that this is a technology that is hugely promising, but as they innovate, they also cannot afford to get it wrong. He said it is essential that AI integration is sustainable and for the betterment of society.

 

“The strong presence of global leaders, especially from the consulting industry, highlights AI’s pivotal role in business transformation and global innovation, and their commitment to collaboration as we seek to resolve the many questions that this technology raises." He said.

– END –