Kuwaleta pamoja zaidi ya viongozi 300 wa Akili Bandia duniani
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUTANO
wa Kimataifa wa Akili Bandia (Global AI 2024) unaoandaliwa na Mamlaka ya ya
Saudia ya Akili Bandia (SDAIA) unatarajiwa kufanyika mjini Riyadh, Saud Arabia
Septemba 10 mpaka 12 huku ukitarajiwa kuwaleta pamoja viongozi zaidi ya 300 wa
akili bandia.
Mkutano
huo unatarajiwa kuwa na moja ya mikusanyiko muhimu zaidi katika Akili Bandia
mwaka huu ambapo jana mamlaka hiyo imetangaza safu yake ya wazungumzaji wakuu.
Taarifa
iliyotolewa Dar es Salaam jana na Balozi wa Saudi Arabia hapa nchini, Yahya Bin
Ahmed Okeish imesema mkutano huo ambao unaenda sambamba na Dira ya Saudi Arabia
ya 2030 inayolenga kuleta uchumi mchanganyiko, umeandaliwa ili kukuza
ushirikiano wa kimataifa na kuangalia uwezekano wa kuleta mabadiliko ya Akili
Bandi katika sekta mbalimbali.
“Mijadala
ya wazungumzaji zaidi ya 300 wakiwemo wavumbuzi, wasomi, watendaji, wadhibiti
na watoa maamuzi kutoka nchi 100 duniani kote itazingatia Kaulimbiu ya mkutano
huo isemayo "Sasa, ifuatayo, Kamwe". Ilisema taarifa hiyo.
Aidha
taarifa hiyo imeelza kuwa vikao vitajadili athari za mabadiliko ya teknolojia
kwa watu na jamii, faida halisi inayopata dunia kutokana na Akili Bandia,
mwelekeo wa teknolojia wa siku zijazo na umuhimu wa kuzingatia maadili ili
kuhakikisha kuwa uwajibikaji wa maendeleo ya Akili Bandia unakuwa katika sekta
zote.
Mkutano
huo utajumuisha safu ya kuvutia ya wazungumzaji wa kimataifa ikiwa ni pamoja na
Cristiano Amon ambaye ni Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Qualcomm
Incorporated, Nick Studer, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Oliver
Wyman Group, Dk. Marc Raibert ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Boston
Dynamics, Marcelo Claure ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Claure Group na Julie Sweet ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
ya Accenture.
Wengine
ni Amandeep Gill, Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Teknolojia,
Kathleen Kennedy ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha MIT cha akili ya
pamoja, Alex Smola ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Boson AI, Andrew
Feldman, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Cerebras Systems, Dk.
Chris Miller, Mkurugenzi wa kampuni ya Greenmantle na Caroline Yap, Mkurugenzi
Mkuu wa Kimataifa kutoka kampuni ya Google Cloud.
Taarifa
hiyo imewataja wengine kuwa ni Stefan Schnorr ambaye ni Waziri wa Nchi
anayeshughulikia masuala Dijitali na Uchukuzi ya Shirikisho la Ujerumani,
Charles-Edouard Bouée, Mwanzilishi Mwenza na Mshirika Msimamizi wa kampuni ya Adagia),
Jonathan Ross ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Groq
na Dk. Deepak Chopra ambaye ni Mwanzilishi wa taasisi Chopra.
Wakati
huohuo Msemaji Mkuu wa Mamlaka ya Saudi Arabia ya Akili Bandia (SDAIA), Mhandisi
Majed Al-Shehri, amesema mkutano wa Kimataifa wa Akili Bandia utakuwa ni tukio
la kihistoria katika kuunda mustakabali wa Akili Bandia na kwamba Kaulimbiu ya
“Sasa, Ijayo, Kamwe” ni muhimu sana kwani inawapa changamoto ya kuangalia
athari za haraka, uvumbuzi wa siku zijazo, na majukumu ya kimaadili yanayokuja
na maendeleo ya haraka ya teknolojia ya Akili Bandia.
“Hii
ni teknolojia ambayo inatia matumaini sana, lakini tunapovumbua, pia hatuwezi
kumudu kuikosea. Ni muhimu kwamba ushirikiano wa Akili Bandia uwe endelevu na
kwa ajili ya kuboresha jamii. Ushiriki mkubwa wa viongozi wa kimataifa, haswa
kutoka katika tasnia ya ushauri unaonesha jukumu muhimu la Akili Bandia katika
mabadiliko ya biashara na uvumbuzi wa kimataifa na kujitolea kwao kwa
ushirikiano katika kipindi ambacho tunatafuta namna ya kutatua maswali mengi
ambayo teknolojia hii inayaibua." Alisema.
-
MWISHO -
No comments:
Post a Comment